Kwa nini mwanangu asome MustLead na sio shule nyingine?

 1. ADA: Mfumo wa malipo ya ada ni chaguo la Unapanga ulipe ada kwa awamu ngapi. Unaweza kulipa kwa awamu 1,2,3,4,5,6,7,8,9 au 10. Unaweza kulipa ada kwa kila wiki pia. Unachagua wewe.
 2. MASOMO YA ZIADA: Wanafunzi wanafundishwa pia Maarifa ya ziada kama vile Kompyuta, Kilimo-Biashara (Matunda na Mboga Mboga), Ufugaji, Sanaa na Michezo n.k.
 3. UFUNDISHAJI WA LUGHA ZA KIGENI: Tunafundisha lugha za Kigeni mf. Kifaransa, Kichina na Kiingereza. Lugha hizi ni muhimu   katika karne hii ya utandawazi.
 4. FEDHA NA VIPAJI: Wanafunzi Wanajifunza Maarifa ya fedha na Maisha, Utambuzi wa Vipaji, Ujasiriamali n.k ili wakimaliza shule waweze kujiajiri.
 5. MFUMO WA MALIPO: Mfumo wa malipo umerahisishwa kweli Mzazi analipa ada popote alipo na wakati wowote kwa kutumia namba maalumu ya mwanafunzi ya malipo (Control Number) akiwa Bank, Kwa Wakala au Kupitia Simu yake ya Mkononi.
 6. TAARIFA ZA MWANAFUNZI: Mzazi anapokea taarifa za Maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma Mf. Majaribio na mitihani ya kila mwezi kupitia simu yake ya mkononi (App) popote alipo. Hivyo kupunguza usumbufu kwa mzazi.
 7. TAALUMA: Shule inafanya vizuri Kitaifa, Kimkoa na Kiwilaya. Mwaka 2020 ilishika nafasi ya kwanza matokeo ya darasa la saba Kiwilaya katika kundi lake.
 8. KIBUBU CHA ELIMU: Mustlead Schools ni shule pekee nchini ambapo kuna mfumo maalumu kwa wazazi wenye kipato kidogo na kisicho na uhakika. Unalipa ada kidogo kidogo kabla ya mhula kuanza au ndani ya mhula. Unaweka kiasi cha fedha yoyote unayopata kwenye kibubu chako unacho-tengenezewa na shule. Utapatiwa risiti ya mashine (EFD) kila unapoweka fedha.
 9. MAZINGIRA Mazingira ya kusoma ni mazuri. Zipo sehemu za wazi wanafunzi kusoma na kufanya mijadala. Shule imejitenga sehemu ya utulivu. Ulinzi niwauhakika.
 10. DINI NA MAADILI: Kila mwanafunzi anapata muda wa kushiriki ibada kwa imani na dhehebu Siku za ibada, Magari ya shule huwapeleka wanafunzi, Waislam Msikitini Siku ya Ijumaa. Wakristo hupelekwa kanisani Wakiwa na walimu wao. Walimu wanasimamia maadili ipasavyo.
 11. WAFANYAKAZI WA KIPEKEE: Shule ina wafanyakazi wenye Upendo. Watiifu na Waadilifu. Wabunifu na Wachapa kazi, ambao wanaishi ndani ya eneo la shule. Zipo nyumba za walimu.
 12. AFYA: Huduma za Afya, Maji na Chakula zimepewa umuhimu wa Wapo Waalimu Wanao simamia afya za wanafunzi. Ipo Zahanati ya karibu. Kuna gari la shule kwa ajili ya wagonjwa masaa 24.
 13. MICHEZO: Kuna viwanja vya Wanafunzi kupitia walimu wa michezo hufanya mazoezi na kushiriki katika mashindano mbalimbali ya UMITASHUMTA na UMISETA. Baadhi ya wanafunzi wamefika hadi ngazi ya mkoa katika mashindano mbalimbali ya michezo.
 14. KUTEMBELEA WANAFUNZI: Kwa wanafunzi wa Bweni, Kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi mzazi anaruhusiwa (akipenda) kumtembelea mtoto Hii hutoa fursa kwa wazazi kuwaona watoto wao kutegemeana na muda wao.
 15. OFA MBALIMBALI: Wenye mtoto zaidi ya mmoja hupewa punguzo la asilimia 5 (5% off) ya ada. Waliomaliza elimu ya msingi hapa kwetu (Mustlead Primary School) na kujiunga na shule ya Sekondari ya MUSTLEAD hupewa punguzo la asilimia 10 ya ada (10% off).
 16. URAHISI WA KUJIUNGA: Piga simu ya shule 0753 211 111 kwa shule ya Msingi na 0713 150 841 kwa shule ya Sekondari. Aidha, Fomu za Kujiunga unaweza kutumiwa kwa njia ya Mtandao au ukafika shuleni moja kwa Unaweza pia kutembelea tovuti ya MUST LEAD GROUP (www.mustleadgroup.com)
 17. BWENI: Huduma za Bweni ni za Kiwango cha juu. Wanafunzi hulala kulingana na umri na Kila Bweni lina walezi wawili kuwahudumia watoto. Aidha, watoto hupewa mafunzo ya maisha ya nyumbani na maadili.
 18. ZAWADI KWA WAHITIMU: Kila mwaka shule hutoa zawadi kwa wahitimu, ikiwemo Tshirts na Vitabu Vya Maarifa Vitabu vilivyotolewa kwa wahitimu hadi sasa ni TETEMEKO LA UJANA (2020), KIJANA MWENYE NDOTO KUBWA (2021) na WHY YOU SHOULD NOT LOSE HOPE (2022).
 19. TUZO: Taasisi imepokea tuzo mbalimbali za Ushindi. Moja ya Tuzo Kubwa ni ile ya Ushindi wa Shindano la Ujasiriamali Nchini kutoka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
 20. USAFIRI WA UHAKIKA: Wanafunzi wa Kutwa huchukuliwa na kurudishwa na gari za shule. Barabara ya Chalinze-Msata, Bagamoyo-Msata, Tanga-Msata gari za shule hupita. Ndani ya kila gari kuna Mwalimu-Msimamizi kwa Usalama wa Watoto